Jeshi la Nigeria limeanzisha operesheni kamambe dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram nchini humo. Makamanda wa jeshi la Nigeria wamesema jana kuwa, operesheni hiyo imeanzishwa kufuatia shambulio la kinyama lililofanywa na kundi la Boko Haram dhidi ya wanachuo wa Chuo cha Kilimo katika eneo la Gujba na kusababisha wanachuo wasiopungua 50 kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa.
Jeshi limetangaza kuwa, jana ilifanyika operesheni mpya ya angani na nchi kavu dhidi ya ngome za kundi hilo katika jimbo la Yobe lililoko kaskazini mashariki mwa Nigeria na kupelekea kuuawa makumi ya wanamgambo wa kundi hilo.
Jeshi la Nigeria limeeleza kuwa, operesheni hiyo ilifanyika kwa mafanikio makubwa dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na wafuasi wa kundi la Boko Haram.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, katika miezi ya hivi karibuni kundi hilo limeshadidisha mashambulizi yake katika eneo la Borno lililoko kwenye mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Cameroon, Niger na Chad.
CHANZO-IDHAA YA KISWAHILI IRAN.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni