Written by Zdaima // 02/10/2013 // Habari // 7 Comments
Ilikuwa ni tarehe 30 Septemba,2013 majira ya saa kumi na mbili kasoro ya jioni. Pale mbele ya Makao Makuu ya KVZ eneo la karibu na eneo la MTONI KISASI kulitokea mkasa huu.
Daladala ya abiria ikitokea mjini kuelekea michungwa miwili nje ya mji,karibu na eneo la makao makuu ya KVZ, ilitokea kubabaishana madereva wa daladala na gari ya KVZ aina ya escudo kiasi cha dereva wa daladala kuikwaruza escodo ya KVZ iliyokuwa inataka kuingia barabarani ikitoka kwenye kambi.
Baada ya hali hio, wale KVZ wakataka kumvamia yule dereva wa daladala na kuzusha taharuki, ndipo yule dereva kuamua kujinusuru kwa kukimbiza gari kuelekea kituo kikuu cha polisi cha bububu nini kilifuata?
Askari wa KVZ waliifukuza ile daladala kwa kishindo kikubwa huku wakipiga risasi hewani ovyo ovyo jambo lililozuwa tafrani kwa wapiti njia, abiria waliokuwemo kwenye gari na wanafunzi waliokuwa wametoka skuli muda huo. Hali ilikuwa ni kama kuna uvamizi wa majambazi na ikawa ni kizaazaa kweli kweli katika barabara hio.
Baya zaidi, wale askari wa KVZ walipofika kituo cha polisi ambapo dereva wa daladala alijisalimisha, wale KVZ walikwenda na kutaka kuwalazimisha POLISI wawakabidhi yule dereva na ikawa ni ubabe tu. Hali ilikuwa ni ya mvutano na sasa ikageuka ikawa ni baina ya KVZ na POLISI. Nilishuhudia baadhi ya POLISI kituoni pale wakirushiana ngumi na maneno makali kwa wale KVZ na ikawa kama ni ugomvi miongoni mwa vikosi vya ulinzi. Hafla umati wa watu ulijaa kituoni hapo na kuzusha masuali mengi.
Watu wengi walikuwa wakijiuliza masuali haya
1, Jee kulikuwa na ulazima wa KVZ kupiga risasi na kuleta taharuki kiasi kile kwa kosa hilo?
2. Ujasiri wa KVZ kwenda kufanya vurugu POLISI wameutowa wapi?
Nami niulize kwa mshangao hivi kama sheria zilikiukwa kwa tukio hili wahusika watachukuliwa hatuwa? mimi nina wasiwasi maana hata TUKIO LENYEWE halikuripotiwa kwenye vyombo vya habari
HII NAYO NI KADHIA WALIOKOSA WACHUKULIWE HATUWA maana sijuwi ingekuwaje kama wale abiria wangelipata ajali maana huo mwendo wa dereva wa dalaladala ulikuwa unatisha wakati akikimbia milio ya risasi za KVZ.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni