Wabunge wa Kenya wanapanga mikakati ya kutoa wito wa kufungwa kambi zote za wakimbizi wa Somalia nchini humo baada ya shambulizi la wiki iliyopita la wanamgambo wa kundi la al Shabab jijini Nairobi.
Mkuu wa Kamati ya Ulinzi ya Bunge la Kenya Ndung'u Gethenji amesema kuwa Kenya inapaswa kutazama upya ukarimu wake wa kuwapa hifadhi wakimbizi ndani ya ardhi ya nchi hiyo.
Inaripotiwa kuwa zaidi ya wakimbizi laki tano wa Kisomali wanaishi katika kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani ya Dadaab. Kambi hiyo iko katika mkoa wa Mashariki. Wakimbizi wengine 30 elfu wa Kisomali wanaishi jijini Nairobi.
Gathenji amesema kuwa baadhi ya kambi hizo zinatumiwa kwa ajili ya kutoa mafunzo.
Septemba 21 mwaka huu watu wasiopungua 67 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa baada ya wanamgambo wa kundi la al Shabab la Somalia kushambulia jumba lenye maduka la Westgate jijini Nairobi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni