Kiwango hicho cha maji ni kidogo ikilinganishwa na maelfu kadhaa ya tani za maji yenye mionzi ya sumu ambayo yamevuja, mengi yake yameingia katika bahari ya Pacifik, tangu lilipotokea tetemeko kubwa la ardhi na Tsunami na kukiharibu kinu hicho mwaka 2011.
Kampuni inayoendesha kinu hicho ya Tokyo Electric Power, imesema jana kuwa wafanyakazi hao waligundua kuwa maji hayo yanavuja kutoka juu ya tangi hilo kubwa wakati wakifanya doria katika eneo hilo usiku juzi.
Tangi hilo ni moja kati ya matangi 1,000 yaliyowekwa katika maeneo ya kiwanda hicho kuhifadhi maji yanayotumika kupooza nishati ya nyuklia inayoyeyuka katika kinu kilichoharibiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni