Habari

Jumanne, 8 Oktoba 2013

Mulatu Teshome achaguliwa kuwa Rais wa Ethiopia

Jumanne, 08 Oktoba 2013 14:05

Mulatu Teshome achaguliwa kuwa Rais wa Ethiopia
Bunge la Ethiopia limemchagua balozi Mulatu Teshome kuwa Rais mpya wa nchi hiyo. Dakta Tedros Adhanom, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ethiopia amewaambia waandishi wa habari kwamba, balozi Mulatu amechaguliwa kuwa Rais mpya wa nchi hiyo akichukua nafasi ya Girma Wolde-Giorgis na ataiongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka sita. Kabla ya kuchaguliwa kuchukua nafasi hiyo, Mulatu alikuwa balozi wa Ethiopia nchini Uturuki. Aidha Rais huyo mpya wa Ethiopia amewahi kuhudumu nafasi ya balozi katika nchi za Japan na China. Balozi Mulatu amewahi pia kuhudumu kama Waziri wa Kilimo nchini Ethiopia. Akizungumza muda mchache baada ya kukabidhiwa ofisi, balozi Mulatu amesema ni heshima kubwa kwake kuchaguliwa kuwa Rais wa nne wa Ethiopa na kuahidi kwamba, atafanya kila awezalo kuiletea maendeleo nchi hiyo. Kwa mujibu wa Katiba ya Ethiopia cheo cha Rais ni cha hadhi na heshima tu na mwenye nguvu na madaraka zaidi ni Waziri Mkuu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni