Na Hanifa Salim, PEMBA.
MWENDESHA mashitaka kutoka Ofisi ya mkurugenzi wa mashitaka Seif Mohamed Khamis, ameiomba mahakama kulipangia shauri la mshitakiwa Nassor Khatib Mbarouk (35) aneshitakiwa kwa kosa la kupatikana na bangi siku nyengine kwa sababu mshitakiwa hakuwepo mahakamani.

Alidai kuwa shauri hilo lipo mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa ingawa hadi anafika mahakamani hapo hajapata habari yoyote ya mshitakiwa huyo na kuiomba mahakama kulipangia tarehe nyengine.
“Mheshimiwa hakimu shauri lipo kwa ajili ya kusikilizwa kwa upande wa mashahidi hatujapokea mashahidi na mshitakiwa hayupo tunaomba shauri hili ulighairishe na kulipangia siku nyengine kwa ajili ya kuskilizwa kwa mashahidi”, alidai Mwendesha mashitaka.Kwa upande wake, Hakimu wa mahakama ya Mkoa wa chake chake Khamis Ramadhan Abdalla alilighairisha shauri hilo hadi Aprili 29 mwaka huu, mshitakiwa atakapo kuja mahakamani hapo na mashahidi watakapo kuja kwa ajili ya kutoa ushahidi.
Awali mshitakiwa alitenda kosa Aprili 20 mwaka 2010, majira ya saa 11:35 usiku, Mzambarautakao Wilaya ya Wete mkoa wa kaskazini Pemba alipatikana na boksi moja la bangi, yenye uzito wa kilogramu 10.5 ambayo ni madawa haramu ya kulevya.
Kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 16 (1), (b) sheria namba 9 ya mwaka 2009 sheria ya kuzuia uingizaji na utumiaji wa madawa haramu sheria ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni