KATIBU Mkuu wa Chama wa wananchi CUF Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, askizungumza na wamachama na CUF kisiwani Pemvba katika mkutano wa hadhara huko katika kiwanja cha Gomabni ya Kale.
MKURUGENZI wa mambo ya nje wa CUF, Issmail Jusa ladu akizungumza na wanachama wa CUF kisiwani Pemba, katika mkutano wa hadhara wa chama hicho huko Gombani kongwe kisiwani Pemba.
NAIBU katimu mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazurouwi akizungumza na wanachama wa CUF kisiwani Pemba, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Gombani Kongwe kisiwani Pemba.
Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CUF akifuatilia kwa makini mkutano huo uliofanyika Gombani ya Kale Pemba.
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharrif Hamad akinguruma katika uwanja wa Gombani ya Kale Pemba.
Na Is-haka
Mohammed,PEMBA.
KATIBU Mkuu wa Chama cha wananchi CUF, Maalim
Seif Shariff Hamad,ameendelea kusisitiza kuwa katiba inayopendekezwa haitaondoa
kero zinazowakabi wananchi wa Zanzibar katika Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.
Maalim Sief
ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema katiba hiyo
inayopendekezwa haina maslahi ya Zanzibar na watu wake,bali ina maslahi na
chama cha mapinduzi CCM ambao waliipendekeza.
Katibu Mkuu
huyo amesema hayo hapo jana katika Mkutano wa hadhara uliandaliwa na chama
hicho katika Uwanja wa Gombani ya Kale na kuhudhuriwa na wanachama wengi wa CUF
na wananchi mbali mbali.
Kupitia
mkutano huyo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar aliwataka wafuasi wa chama
hicho na wananchi kwa ujumla kutoyatilia maanani maneno ya watu wanaopita
wakifanya mikutano kuwa katiba hiyo imeondosha kero zote zinazowakabili
Wazanzibari kwa kusema ni uzushi mtupu.
Ameifananisha
katiba hiyo ni sawa na kifaru mwenye uzito wa kilo 100 na kutolewa kichwa chake
chenye uzito wa kilo 10 kuwa itakuwa kifaru huyo hatoweza kuishi.
“Ngugu zangu
wananchi msingi wa katiba hii umeondolewa hivyo haifai na wala haina maslahi na
sisi wanzibar kwa vile msingi mkuu umeondoshwa katika katiba inayopendekezwa
ambayo ni serikali tatu”alisema maalim Seif.
Kwa upande
mwengine amesema Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar inapaswa kuwa na sheria na sera madhubuti, zitakazotumika katika
uzalishaji wa rasilimali za Mafuta na Gesi Zanzibar.
Maalisef amesema kuwa, Serikali haipaswi kukurupuka
katika uvunaji wa rasilimali ya Gesi na Mafuta, pasi na sheria na sera
madhubuti, kwani baada ya kutaka manufaa inaweza ikaleta balaa kwa wazanzibari.
Amefahamsiha
kuwa Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar, kwa sasa haina sera wala sheria yoyote
ya mambo ya mafuta na Gesi, jambo ambalo halifai kisheria.
Amesema kuwa
pindi pakiwepo na seri na sheria nzuri zitakazoweza kuwanufaisha wazanzibari,
Zanzibar isije ikarudia makosa yaliyofanywa na baadhi ya nchi za Afrika baadae
kupigana wenyewe kwa wenyewe juu ya mafuta na rasilimali nyengine.
Aliishauri
Serikali kuunda chombo maalumu ambacho kitasimamia masuala hayo ya mafuta na
gesi Zanzibar, kama ilivyo Tanzania bara kwa lengo la kuwepo na usimamizi
madhubuti, juu ya masuala hayo ili wazanzibari wenyewe waweze kunufaika na
rasilimali hiyo.
Akizungumzia
suala la rasimu ya mpya ya katiba iliyokabidhiwa kwa Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar, amesema kuwa rasimu hiyo haikuonyesha
heshima ya Rais kikwete na kutokufikia lengo lililokusudiwa, la kuwakomboa
wananchi na umasikini, pamoja na kuondosha kasoro zilizokuwa zikipigiwa kelele
na wananchi.
Amesema kuwa
rasimu ya katiba iliyopendekezwa inakwenda kinyume na matakwa ya wazanzibar,
kwani mambo ambayo wazanzibari wameyataka na kuyawasilisha katika tume ya Jaji
warioba yametolewa na kuwekwa mengine.
Hata hivyo
amewapongeza wabunge wa Umoja wa katiba ya wananchi Tanzania “UKAWA”,kwa
msimamo wao kutetea amani ya wananchi katika masuala mbali mbali.
Kwa upande
wake Naibu katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazruwi amesikitishwa kwa
kuondolewa maoni yote ya wananchi waliyoyapendekeza katika rasimu ya katiba ya
Jaji Warioba na kuingizwa mawazo ya wenngine.
Alisema kuwa
wazanzibar wanataka mamlaka yao kamili katika rasimu hiyo, kwa lengo la
kujiamulia mambo yao wenyewe ili waweze kujenga nchi yao.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni