Katika utafiti huo zimeunganisha Shehia 80 za Zanzibar ambazo zitashirikisha nyumba 350 ambapo kila Shehia itawakilishwa kwa nyumba 5, ambapo utafiti huo utaanza Septemba 10 hadi Novemba 26 mwaka huu.
Mtafiti Mkuu wa mpango huo Dk. Antje Haebestreit kutoka Chuo kikuu cha Breen nchini Ujerumani, alisema lengo la utafiti huo ni kuisaidia Serikali na jamii katika juhudi kupunguza matatizo ya kiafya yatayowakabili kutokana na ukosefu wa lishe bora.
Akizungumza katika mkutano wa utafiti wa usalama wa chakula na lishe juu ya upatikanaji vyakula na hadhi ya lishe kwa wazanzibari hoteli ya bwawani alisema, katiika utafiti huo wananchi pia watafanyiwa vipimo vya damu, kisukari na presha.
“Katika utafiti huu endapo wananchi watagundulika katika kupimwa vipimo hivyo na kugundulika maradhi yakiwemo unene na uzito wa kupindukia watapatiwa tiba kupitia taasisi na serikali ili waondokane na matatizo yanayowakabili” alisema Dk. Antje.
Pia ameongeza kuwa watahamasisha masheha kuelewa umuhimu wa ushiriki katika utafiti huo na kujua hali halisi ya lishe na usalama wa chakula kwa afya za Wazanzibari ili kutoa taaluma hiyo kwa wananchi.
Dk.Antje alisema watashirikiana na Serikali kupitia Wizara ya afya kwa kuitatafuta njia mbadala ya kutatua shida zao ama kutafuta wafadhili.
Nae Profesa Mohammed Ali Shehe kutoka SUZA, alisema wananchi watanufaika baada ya utafiti huo kugundua na kupata majibu watawasiliana na serikali na wadau wa tafiti pamoja na wadau wa afya na serikali ambapo watakuwa katika kutoa huduma kwa wananchi wa Zanzibar.
Amewataka watafiti wa ndani kujikita zaidi katika tafiti za matatizo ya jamii pamoja na kuimarishwa maabara ama taasisi za kitafiti ikiwemo vifaa vya kisasa ili kuweza kugundua matatizo haraka kwa binadamu.
Kwa upande wa Profesa Sorge Kelm, kutoka chuo kikuu cha Bremen, Ujerumani, ameiomba serikali kutoa ushirikiano ya karibu katika kuunga mkono katika kuendesha utafiti huo na pamoja na masheha kujenga mashirikiano na jamii katika kufanya utafiti huo na kuweza kufanikisha utafiti wa chakula na lishe.
Nao masheha wametoa wito kwa taasisi hiyo kuwashirikisha watu wenye ulemavu wa akili kuwapa elimu hiyo ya lishe ili kupata uwelewa na kushiriki katika zoezi hilo.
Dk. Antje alisema mradi huo wa utafiti wa upatikanaji wa vyakula na hadhi ya lishe kwa wazanzibar na umeandaliwa na watafiti kutoka Vyuo vikuu vya SUZA na Bremen.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni