WILAYA YA CHAKE CHAKE.
BARAZA LA MJI wa Chake Chake limepokea
msaada wa vikapu vya kuzolea taka pamoja na magari mawili ambayo ni msaada
kutoka bank ya dunia kupitia serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Hayo yameelezwa
na katibu wa Baraza hilo Nassor Suleiman Zaharani wakati akizungumza na Sauti ya Istiqama huko
ofisini kwake Chachani Chake Chake.
Amesema msaada
huo utasaidia sana katika kuweka usafi
katika maeneo mbali mbali ya mji huo
kwa vile kabla walikuwa wakipata upungufu mkubwa kwa kukosa vitendea
kazi jambo ambalo lilikuwa likikwamisha kazi zao za kila siku.
Amesema msaada huo ni muhimu kwa wakati huu kwani
utasaidia kuimarisha usafi katika maeneo tofauti ya mji kwa vile baraza limeshaanza kuvisambaza vikapu hivyo katika
maeneo ambayo yana tatizo ya sehemu za kuhifadhia taka.
Hata hivyo
katibu huyo amewataka wananchi kuvitumia vikapu hivyo kwa kuhifadhia taka kwa
kuzitia ndani yake na wasizitupe chini ya vikapu hivyo kwani husababisha
kusambaratika ovyo jambo ambalo hupelekea kuongezeka kwa uharibifu wa
mazingira.
Katibu huyo
wa Baraza la mji amesema changamoto kubwa inayowakabili ni vikapu hivyo
kubakisha taka wakati wa umwagaji,huku akiomba msaada zaidi wa magari ili
kuweza kumudu vizuri katika kuweka mandhari ya mji huo vizuri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni