NaIs-haka Mohmmed,Pemba. Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Sada Mkuya
Salum amesema kukamilika kwa ujenzi wa barabara tano katika mkoa wa Kaskazini
Pemba kutanyua uchumi wa wananchi wa maeneo husika.
Akizungumza
mara baada ya kutembelea barabara hizo zinazojengwa na kwa msaada wa Serikali ya Marekani kupitia
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amewataka wananchi hao kuzitumia
barabara hizo katika kujikwamua na umaskini.
Amesema
kutokana na ujenzi wa barabara hizo tayari mabadiliko yameshaanza kuonekana kwa
wananchi wa maeneo husika ikiwemo kusafirisha mazao yao kwa njia ya urahisi.
Kwa upande wake
Mbunge wa jimbo la Ole Rajabu Mbarouk Mohammed
ameipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzijenga
barabara hizo katika kiwango chenye ubora wa hali ya juu.
Amesema
barabara hizo zitasaidia kupunguza changamoto mbali mbali zilizokuwa
zikiwakabili wananchi wanaoishi katika maeneo hayo,kwa kuwapa urahisi katika
usafiri hasa wagonjwa.
Akizunguzia
hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa barabara hizo, Mhandishi wa mradi kutoka
serikali ya Zanzibar Joseph Malambi amesema ni nzuri na ujenzi utakamilika
katika wakali uliopangwa wa mwezi Disemba.
Barabara
hizo ni Mzambarau Takao-Pandani, Bahanasa-Daya Mtambwe, Mzambarau Karim-Wingwi
Mapofu, Chale- Kojani na Amani road- Kangagani zote zikiwa na urefu wa kilomita
35.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni