PEMBA. Wananchi waliokuwa hawakubahatika kupata elimu walipokuwa wadogo wana
fursa kubwa ya kutumia vituo vya elimu ya watu wazima na madarasa ya elimu
mbadala kujiendeleza kielimu na kuondokana na tatizo na ukosefu la idadi kubwa
ya wananchi wasiojua kusoma na kuandika,
Hayo
yameelezwa na Mratibu wa Idara ya Elimu ya watu wazima Pemba Mw. Hija Hamad
Issakatika Siku ya Juma la Elimu Duniani ambapo kwa upande wa Mikoa miwili ya
Pemba zimeadhimishwa huko katika Skuli ya Madungu Sekondari Chake Chake.
Amesema
kupitia elimu ya watu wazima wananchi waliokosa kupata elimu wakiwa wadogo na
wale walioshindwa kuendelea na masomo ya juu wanaweza kupata elimu na kujiari.
Aidha Afisa
huyo elimu ya watu wazima amewashajihisha kina mama kujiunga katika madara ya
elimu ya watu wazima sambamba na kuanzisha vikundi vya ushirika vya uzalishaji
mali ili kujiendeleza kiuchumi.
Kwa upande
wake mgeni rasma katika ghafla hiyo Afisa Mzamini Wizara ya Katiba na Sheria
Mw. Omar Khamis amesema elimu ina umuhimu mkubwa kwa taifa lolote lile katika
kufikia maendeleo,pia inatoa mwanga wakujikomboa
katika uzalishaji mali, kuondokana na ujinga,maradhi na umaskini.
Amesema kuwasaidia
vijana na watu wazima kupata elimu na kuishi vizuri ni kulisaidia taifa katika
kufikia maendeleo yake na kuondokana na watu wategemezi katika kila kitu.
Ikiwa Idara
hiyo inatimiza miaka 34 tokea kuanzishwa kwake tayari ina vituo vya kisomo 59
na madarasa 141 kisiwani Pemba,ambapo wanakisomo 3541wanawake na wanaume 3285
wanashiriki katika kisomo na vijana 421 wamejiandikisha katika madarasa ya
elimu mbadala katika mikoa miwili ya Pemba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni