Habari

Jumanne, 1 Oktoba 2013

KWA SABABU YA WOGA WA WAKAZI WAKE KUSILIMU, MEYA AGOMA KUTOA KIBALI CHA UJENZI WA MSIKITI

Meya wa mji wa Moscow Sergey Sobyanin  amesema mji wake hauna mpango wa kuruhusu tena ujenzi wa msikiti mpya kwani kwa kufanya hivyo kuna madhara kwa wakazi wenye asili na mji huo, aliyasema hayo wakati akihojiwa na kituo cha redio cha echo Moscow.


Alisema Wengi wa waislamu wa mji wa Moscow ni wahamiaji waliokuja kufanya kazi. Na kwamba kuna asilimia 10 tu wakazi waislamu hivyo haoni kama kuna haja ya Kuruhusu ujenzi wa msikiti mwingine mpya.

Aidha anakasirishwa na watu hao wanaozungumza lugha tofauti, tabia tofauti pamoja na tabia ya 'fujo', kuanza kuigwa na wakazi wenye asili ya mji huo na uingiaji wa kasi katika dini ya kiislamu kwa wakazi wa Moscow kuna madhara kwa baadae.

Alisema kuna wafanyakazi wahamiaji 200,000 na asilimia 35 kati yao ndio wenye ujuzi. Meya huyo alisema ni muhimu kupunguza sehemu ya wafanyakazi wasio na ujuzi.

Kulingana baadhi ya makadirio ya Moscow kuna mhamiaji mmoja haramu katika wahamiaji 10 waliosajiliwa. Hii inafanya idadi ya wafanyakazi wa kigeni waliosajiliwa katika mji huo kufikia milioni mbili. Mwaka 2012 mamlaka ya Moscow iliwafukuza wageni 16,000 kwa kosa la kufanya kazi kinyume cha sheria.

Hata hivyo Kauli ya Meya huyo imepingwa vikali na waislamu wa nchini urusi kwa kusema mahitaji ya ujenzi wa msikiti ni makubwa kulingana na wingi wa waislamu nchini humo ambapo inawalazimu kusali Barabarani.

Makamu mwenyekiti wa baraza la Mufti wa Russia Nafigulla Ashirov alisema waislamu hawakubaliani na meya huyo na kwamba wanapeleka maombi yao kwa Rais Vladimir Putin kwa msaada zaidi. Russia ni mojawapo ya nchi zinazokabiliwa na wimbi kubwa la ukuaji wa dini ya kiislamu.

Waislamu wakisali Eid El fitr mwaka huu huko Moscow

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni