Zaidi ya miili tisa imepatikana kutoka vifusi vya jengo hilo, miili mingine ikiwa imeharibika kutokana na moto mkali ambao uliteketeza sehemu ya jengo hilo.
Baadhi ya duru za polisi zimesema kuwa baadhi ya miili haiwezi kutambulika na inahitaji uchunguzi wa vinasaba DNA kuweza kuitambua.
Hata hivyo haijafahamika iwapo miili hiyo iliyopatikana imejumuishwa katika idadi ya watu 67 waliofariki katika shambulio hilo, ama ni miongoni mwa watu 39 wanaohofiwa kuwa hawajulikani waliko.
Wakati huo huo kundi la al-Shabaab la Somalia limetishia leo kuwa litaongeza mashambulio yao dhidi ya Kenya , baada ya serikali kusema haitaondoa majeshi yake nchini Somalia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni