Saturday, October 12, 2013
Na Mwajuma Juma
TIMU ya Soka ya Mtende Rangers imefanikiwa kuwa kinara wa ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt baada ya kuifunga Polisi mabao 2-1 na kufikisha pointi 16 katika msimamo wa ligi hiyo,iliyoendelea juzi visiwani Zanzibar.
Mchezo huo ulichezwa katika viunga vya MaoTse Tung mjini hapa, ulionekana kuanza kwa ushindani mkali katika dakika zote 90 za mchezo huo.
Katika mchezo huo timu zote mbili ziliuanza kwa kasi hali iliyotowa burudani tosha machoni mwa mashabiki waliohudhuria mchezo huo.
Ilichukuwa dakika 28 tu kwa maafande hao wa Polisi kuandika bao la kuongoza lililofungwa na Khalid Kheir nakusawazishiwa dakika tatu baadae kupitia kwa Yahya Said Tumbo na kuwafanya waende mapumziko wakiwa nguvu sawa ya bao 1-1.
Kuanza kwa kipindi cha pili kila timu ilijaribu kufanya mabadiliko ili kuweza kuongeza nguvu kikosi chake lakini mabadiliko yaliyofanywa na Mtende Rangers yaliweza kusaidia kufanikiwa kupata bao la pili na la ushindi katika dakika ya 87 lililofungwa tena na Yahya Said Tumbo.

CHANZO- http://www.zanzinews.com/
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni