12 OCTOBER,2013 Ulevi, starehe za wanawake, kuchati kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo ‘Face Book’ mpaka usiku wa manane ndio chanzo cha Kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni kugombana na wachezaji wake kiasi cha kuchukiwa.
Akizungumza Makao Makuu ya klabu ya Simba jana, Kibadeni alisema anachoshwa na tabia ya wachezaji wanaokuwa na wanawake watatu watatu huku wakiendekeza starehe na ulevi na kuwaonya kujua mpira isiwe sababu ya utomvu wa nidhamu.
“Wachezaji wakipata pesa wanataka watumie watakavyo, wawe na wanawake watatu watatu, walewe, wachati mpaka usiku wa manane, sasa mimi ikifika saa nne nazima taa nawaambia kulala hicho wao hawakitaki, wananivizia nimelala wanawasha taa wanaendelea na mambo yao.
“Kujua mpira isiwe sababu ya kusumbua watu, kuna wachezaji hawajitambui ni lazima tuwaelimishe wengine ni darasa la saba mpira una muda wake asipofanya kitu cha maana leo siku za mbeleni utaishije ni lazima umwuelimishe umepata pesa weka beanki achana na starehe, baba yako umemnunulia nini mpaka utumie hela kwa mambo ya wanawake ndio ninachofanya sasa hiyo wachezaji hawataki.
“Kuna mshambuliaji nimempa mechi saba, hajafunga goli hata moja sasa mimi mnataka nifanyaje? Ni lazima akae benchi Simba tuna wachezaji 36 anayefanya vizuri ndio anayeingia kambini kujiandaa na mechi inayokuja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni