Habari

Jumapili, 27 Aprili 2014

TAIFA stars yapata kocha mpya

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza rasmi Mart Nooij kutoka Uholanzi kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya Taifa (Taifa Stars).
Rais wa TFF, Jamal Malinzi akimtambulisha kocha huyo leo (Aprili 26 mwaka huu)  katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam amesema anafurahi kumtangaza Nooij na anatarajia  Tanzania itanufaika na uzoefu wa  kocha huyo hasa katika bara la Afrika.
 Nooij kabla ya kupewa mkataba huo wa kuifundisha Taifa Stars alikuwa na klabu ya St. Georges ya Ethiopia pia amewahi kufundisha  katika nchi za Burkina Faso, Mali na Msumbiji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni