Habari

Alhamisi, 15 Mei 2014

Madawa ya Kulevya Yahamia Vijijini.

LICHA ya juhudi zilizochukuliwa na  Serikali  kusaidia kupambana na utumiaji wa madawa ya kulevya,bado juhudi hizo hazijazaa faida kutokana na vijana wengi hasa walioko vijijini kuendelea kutumia madawa hayo.


Akizungumza na Zenj FM  Muhamsishaji Mkuu wa Nyumba za kurekebisha tabia kwa vijana walioacha dawa za kulevya(Soba Hause  kutoka JUKAMKUM  Moh’d Rizik Moh’d amesema kuwa katika muendelezo wa utoaji wa elimu kwa vijana hao, kumekuwa na mvutano mkubwa kati yao na wale walioacha kutumia madawa hayo.


Moh`d anayetambulika zaidi kwa jina la ZORO ameelezea kusikitishwa kwake na baadhi ya watu wanaosimamia Sober Hause, kwa kupinga kuwepo kwa mashirikiano na kusababisha kuwepo kwa migogoro baina ya wasimamizi wa nyumba hizo.

Amesema kwa kiasi kikubwa janga la utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana limeonekana kupungua katika maeneo ya mjini lakini nimeanza kushika kasi katika meneo ya ng`ambo na vijijini.

Naye kwa upande wake Kombo Juma Kombo ambaye pia ni muhamasishaji amesema kuna changamoto nyingi  ambazo wanakabiliana nazo ikiwemo ukosefu wa vitendea kazi ambavyo  huwapa ugumu wakati wa utoaji wa elimu.

Sambamba na hayo  wameiyomba srikali kutilia mkazo juu ya kuzisaidia soba hause  kujikwamua na  maisha pia  na kuwataka vijana kubadilika kwa kuachana na  utumiaji madawa ya kulevya 


Nyumba hizo za kurekebisha tabia kwa vijana waliomua kuachana na madawa ya kukevya, zimekuwa na mafanikio ya kuwatoa vijana katika dimbwi la utumiaji wa dawa za kulevya,hata hivyo chanyamoto kubwa na pale vijana hao wanapotoka katika nyumba hizo kutokuwa na shughuli za kufanya.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni