Habari

Jumatano, 11 Septemba 2013

Pemba.
Jamii imetakiwa kuwaelimisha vijana muhimu wa afya ya uzazi ili kutambua na kuepukana na matatizo mbali mbali yanayosababishwa na afya ya uzazi.

Akizungumza na Sauti ya Istiqama, Mratibu wa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania, (Umati)Pemba Maalim Rashid Abdalla Rashid amesema kuwa Afya ya uzazi ni muhimu kwa jamii.
Amesema umuhimu wake ni pamoja na kuepukana na mambo tofauti yanaweza kusababisha madhara kwa mtu, familia na taifa  kwa ujumla.   
Amesema kutokana na vijana kukosa kupata afya ya vijana kumekuwa kukipelekea vijana wengi kujitumbikiza katika masuala ya ngono wakiwa wadogo sambamba na utumiaji wa dawa za kulevya.   
Hata hivyo amesema hili linaweza kufanikiwa zaidi kwa wazazi kuwa na uangalizi mzuri na kukaa na watoto wao kuwaeleza athari za kujiingiza katika matendo hayo.

Hata hivyo, Maalim Rashid amewahimiza wazazi kuwalea watoto wao katika malezi bora yatakayowaepusha na masuala ya uasharati, na utumiaji wa dawa za kulevya na kusema, ndio chanzokikuu  cha kujiingiza katika masuala ya  maambukizi  ya virusi vya ukimwi.
                            MWISHO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni