Wananchi wa
shehia za Mbuguani na Changaweni Wilaya ya Mkaoni wamefika katika ofisi za
Mamlaka ya Maji zilizopo Machomanne wakilalamika kubadilishwa machine ya maji
katika kisima wanachotegemea kupata maji na badala yake kuikosa huduma hiyo kwa
muda sasa.
Wakizungumza
kabla ya kufika katika ofisi hizo na kuonana na wahusika kupeleka kilio
chao,baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa kilichowapeka ofisini hapo ni kutaka
kujua sababu iliyopelekea kukosa maji licha ya kuwekewa mashine mpya na mbunge
aliyepita.
Said Juma ni
mmoja kati ya wananchi hao ambaye amesema wamepatwa na wasiwasi kuwa mamlaka
hiyo ilibadilisha mashine hiyo na ndiy ikawa sabanu ya kukosa maji.
Hata hivyo
kwa upande wake Juma Khamis Issa Mkaazi wa Changaweni Mkoani amesema inatia
shaka kwa Mamlaka ya maji ambaye imeboreshwa kutujua taarifa za matatizo ya
maeneo yao wanayotoa maji.
Amesema
kunaoneka katika mamlaka hiyo hakuna mawasiliano mazuri katika utendaji kwani
wao kabla ya jana kufika katika ofisi kuu za ZAWA Pemba tayari walikuwa wameshatoa
taarifa za tatizo hilo kwa afisa wa ZAWA Wilaya ya Mkoani.
Mwananchi
huyo ameeleza ili mamlaka ya maji iendane na maboresho iliyokusudia ni vizuri
kuwa wafuatiliaji wazuri katika kujua matatizo yanayowakabili wateja wao.
Hata hivyo
walipotoka katika kikaona Mkurugunze wa ZAWA Pemba wananchi hao wamesema
wamezungumza vizuri na wamekubaliana kuwa tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi
haraka.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Pemba Omar Bakar Mshindo licha ya kukiri
kuwepo kwa tatizo hilo lakini amedai kutokuwa na taarifa ya wananchi kukosa
maji kwa muda mrefu.
Amewaeleza
wananchi hao kuwa mashine iliyowekwa na mbunge bado ipo isipokuwa mota ndiyo
iliyoungua na kuamua kuibadilisha na kusema kuwa kukosa huduma ya maji wa
wananchi hao haitokani na tatizo la mashine wala mota.
Hata hivyo
amesema leo au kesho atawapeleka mafundi ili kwenda kuona ni tatizo gani
linalosababisha kukosekana kwa maji katika kisima hicho, lakini pia akieleza
kuhusu kisima hicho ni cha zamani na ni kidogo sana jambo linalopelekea
uzalishaji wa maji kuwa mdogo.
Aidha
amesema hatua madhubuti zinachukuliwa za kuondosha tatizo la maji safi na
salama kwa wananchi ikiwa ni pamoja na mradi wa maji mijini katika miji mitatu
ya Pemba.
Ni zaidi ya
miezi miwili sasa wananchi wa Shehia hizo wamekosa huduma ya maji ya bomba na
kulazimika kufuata maji katika visima pamoja na mito hata hivyo wamesema hayako
salama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni